- Mohamed Morowa
SUBIRA HUVUTA KHERI
Updated: May 13, 2018

Mwanangu matamanio, yasikupe bumbuazi Na sudi ya mwendanio, silalie mwango wazi Mola ndiye tegemeo, mwingine wala hawezi Subira huvuta kheri, usende mwendo wa mbango
Huvuta kheri subira, mwendo wa mbango usende Ni mwendo wenye khasara, wawate wao waende Mwisho watawa majura, wabaki shingo upande Subira huvuta kheri, usende mwendo wa mbango
Beti tatu kwako tosha, uyashike ya mjomba Moyo wako furahisha, mema kwako iwe kamba Hayana wema maisha, abudu wako Muumba Subira huvuta kheri, usende mwendo wa mbango
13 views1 comment