- Hassan Morowa
NI KIPI HAKISHIBISHI?
Chakula gani huliwa, lakini hakishibishi Kukila wajisumbuwa, hata kingi hakitoshi Kukipapia si dawa, simlaumu mpishi Ni kipi hakishibishi?
Msiseme ni haluwa, mwajisumbua bileshi Wala msambe ni muwa, usopikwa na mpishi Ni chakula cha kuliwa, msiulete ubishi Ni kipi hakishibishi?
Nataka lala Morowa, jibu halinikesheshi Kesheni mkiinuwa, vichwa vichoke chokeshi Kiamka tachunguwa, nione uwasilishi Ni kipi hakishibishi?
Jirani wakilemewa, walio Tanga na Moshi Wauzane "man huwa", kisha anauza " "eshi" Waambiwe ni Morowa, yule mzee mcheshi Ni kipi hakishibishi?

56 views0 comments