Je, unajua kwamba dini ya Waswahili kwa kiasi kikubwa ni Uislamu? Je unajua kwamba kuna misamiati kadha wa kadha ambayo inatumika wakati wa Ramadhani pekee? Unaijua? Leo nauliza maswli 10 ya Kiswahili kuhusu Ramadhani. Hebu jichangamshe bongo kidogo kwa kuyajibu hapa chini......


1) Huu ni mwezi wa Ramadhan. Je ile miezi mingine kumi na moja huitwaje kwa ujumla kwa Kiswahili?
2) Je, muislamu ambaye anafaa kufunga lakini akavunja miko yote akawa hafungi mchana wa Ramadhani huitwaje?
3) Mtu akisema ”LEO NIMESHIKWA NA SAUMU” huwa anamaanisha nini?
4) Chakula cha mwisho mtu anachokula kabla kuanza kufunga chaitwaje?
5) ”Kufungua muadhini” ni nini? Na kama kuna ”kufungua muadhini” je, kuna "kufunga muadhini?”
6) Nini maana ya BEMBE?
7) Swala ambayo inaswaliwa wakati wa Ramadhani peke yake inaitwaje?
8) Kile kitu kigumu kinachopatikana ndani ya tende baada ya mtu kumumunya chaitwaje?
9) Neno lililo na maana sawa na KIU ni lipi?
10) Mtu akiwa na ukata ukazidi sana (mpaka ikawa ni kama ni lazima asaidiwe) huyo huitwaje?