MALKIA FORUM

Lets talk photos. But since we don't live in isolation, other topics of interest are welcome but moderated with decorum

PHOTOGRAPHY ISSUES

Lets talk photos. Lets talk passport photos, lets talk Studio Business
 Views
0Posts

MASHAIRI

Tunakaribisha mashairi na pia uhakiki wa shairi au Diwani yoyote ile.
 Views
1Posts

UBINGWA WA LUGHA

Hapa ni pa Umbuji na Ulimbwende wa lugha. Maneno yatumikayo kimakosa, yaliyopotea na njia za kukijenga Kiswahili
 Views
1Posts

TRAVEL ESCAPADES

Interesting places in the world through the eyes of independent visitors. Tell us about your County
 Views
1Posts

LIFE TIPS

Tell us what can add value to our lives. Don't wait for us to make the mistakes, give us life tips
 Views
0Posts

CONSTRUCTIVE POLITICS

What ails our politics, what should we do to better our politics. Lets discuss issues constructively-COUNTY and COUNTRY
 Views
2Posts

RELIGIOUS TOPICS

This is a section dedicated to topical issues with religious tinge
 Views
0Posts
New Posts
 • Hassan Morowa
  Mar 6

  The Kenyan passport is ranked number 72 by the trusted Henley & Partners who assess passport strength by among other variables, the ease of travel worldwide. According to them Kenyans can visit 71 countries in the world without the VISA requirement. The most widely accepted passport is that of Japan where their nationals can visit over 190 countries without a VISA. The worst is Iraq and Afghanistan where nationals of the two countries require VISA to all countries except 30. Normally, whenever you need a VISA to travel, you need a passport size photograph and each country has its own size. Visit Malkia Digitech Studios for the cheapest and best VISA photos in Nairobii CBD. We open from 6.30am daily.
 • Hassan Morowa
  May 27, 2018

  Je, unajua kwamba dini ya Waswahili kwa kiasi kikubwa ni Uislamu? Je unajua kwamba kuna misamiati kadha wa kadha ambayo inatumika wakati wa Ramadhani pekee? Unaijua? Leo nauliza maswli 10 ya Kiswahili kuhusu Ramadhani. Hebu jichangamshe bongo kidogo kwa kuyajibu hapa chini...... � � 📷Want to add a caption to this image? Click the Settings icon. 1) Huu ni mwezi wa Ramadhan. Je ile miezi mingine kumi na moja huitwaje kwa ujumla kwa Kiswahili? 2) Je, muislamu ambaye anafaa kufunga lakini akavunja miko yote akawa hafungi mchana wa Ramadhani huitwaje? 3) Mtu akisema ”LEO NIMESHIKWA NA SAUMU” huwa anamaanisha nini? 4) Chakula cha mwisho mtu anachokula kabla kuanza kufunga chaitwaje? 5) ”Kufungua muadhini” ni nini? Na kama kuna ”kufungua muadhini” je, kuna "kufunga muadhini?” 6) Nini maana ya BEMBE? 7) Swala ambayo inaswaliwa wakati wa Ramadhani peke yake inaitwaje? 8) Kile kitu kigumu kinachopatikana ndani ya tende baada ya mtu kumumunya chaitwaje? 9) Neno lililo na maana sawa na KIU ni lipi? 10) Mtu akiwa na ukata ukazidi sana (mpaka ikawa ni kama ni lazima asaidiwe) huyo huitwaje?
 • Hassan Morowa
  May 27, 2018

  Sijibujibu kidubu, kiwa sina la kujibu Kujibu tajibu jibu, endapo jibu lasibu Lasibu miye najibu, halisibu silijibu! Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu! Mshairi anasema hajibujibu kidubu kiwa hana la kujibu. Kidubu ni ”kama dubu” na dubu au "kakadubu" hutumiwa kuashiria mjinga uswahilini. Yeye hujibu iwapo hilo jibu lasibu. Kusibu ni kutokea jambo kama lilivyosemwa Silijibu nakutubu, kiwa ni la kakadubu Kakadubu simjibu, hapo mimi nitaghibu Nitaghibu bil-ghibu, mwambe 'hini ni ajabu!" Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu Mshairi anahimiza kuwa hajibu na hilo analiandika lionekaniwe wazi. Maadamu ni jibu la kifala yeye ataghibu.Kughibu ni kupotea, kama ambae hayupo. Na atapotea bil-ghibu, Hii ghibu ya pili ni kupotea kwa moyo. Ajabu ni kuharibu, kujibu kama shababu Shababu ataghilibu, au alete ghadhabu Ghadhabu ndani kwa jibu, heri ukawa ghaibu Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu Kivyake, kupotea isiwe ajabu kabisa kwenu kwa sababu ndivyo ifaavyo haswa. Ambalo halifai ni kujibu na katika huko kujibu ukaharibu kama vijana wa leo ambao ni desturi yao kudanganya ili waonekane wajua au walete hasira. Ikifika hapo heri awe ghaibu, awe mbali kuliko kujibu. "Ghaibu" ni kiarabu, "mbali" huwa ndio jibu Jibu lisiwe harabu, na si yangu mat'lubu Mat'lubu ni kujibu, mambo kwa us'tarabu Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu Neno la ghaibu ni Kiarabu linalomaanisha mbali, kutoonekana, kutokuwepo. Asema kuliko kutoa jibu ambalo halifai heri akae mbali na kufanya hivyo sio mat’lubu, anavyopenda. Anavopenda yeye ni kujibu kwa ustaarabu kama inavyotakikana si kupayuka ovyoovyo Us'tarabu si tabu, kwa watu wenye majibu Majibu ya malabibu, ni sawa kwa al'babu Al'babu kuwajibu, huwa wapata thawabu Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu Na kujibu kwa wema si shida kabisa kwa wale walio wajuzi, werevu. Na majibu ya werevu huwaingia akilini wenye akili. Na kufanya hivyo ni thawabu haswa kwa sababu utakuwa umeeneza ilmu ya faida. Thawabu hazitosibu, kijibu ja majdhubu Majdhubu kama zebu, ng'ombe na mtu kidhabu Kidhabu kutowajibu, ndio dawa mjarabu Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu Muandishi aonya kuwa mtu hapati thawabu akijibu kama mwehu aliyemumithilisha na ng’ombe na mwenye kutumia uwongo anapojibu. Watu waongo heri kuwanyamazia Mjarabu matibabu, kwa watu waso adabu Adabu kiwa meghibu, sijibu kajipa tabu Tabu ndan'ni habibu, nenda kaimbe tarabu Si kila swali najibu, mangine si ya kujibu Mshairi anamalizia kuwa Si muongo tu wa kumnyamazia bali hata mkosa adabu mana kumjibu ni kujisumbua bure, Na kwa nini ujisumbue? Heri ukatafute mengine ya kufanya kama kuimba taarabu na kadhalika. Si kila uulizwalo unafaa kulijibu. Saa zingine ni bora kunyamaza kimya ©2014 HASSAN MOROWA "Maji ya Mvua" Nairobi. '''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''' Utagundua kuwa shairi hili limetumia mbinu ya mtiririko maana kila mshororo umejikita katika kina cha "BU" mwanzo na mwisho. Fauka ya hilo, shairi hili ni la pindu, Na hiyo pindu imeendelezwa si kwa mshororo tu bali hata ubeti kwa ubeti. Washairi wengi huukwepa mtindo huu maana ni mgumu ikiwa mtunzi hana msamiati wa kutosha. Kwa kifupi, mtunzi anawashauri watu wasijibu kila swali linaloulizwa kwa sababu maswali mengine ni ya kipuuzi na unapojibu hutokuwa tafauti na mwehu. Huenda ukatukanwa kwa sababu maswali mengine huulizwa kutega watu waseme ili wakosewe hishima na si kwa ajili ya kutafuta taaluma.

© 2018 Designed by Malkia Digitech.

AL-YUSRA  RESTAURANT Bldg.

Banda Close

Opposite McMillan Library

Near Nation Centre

P. O. Box 18780 00100

Nairobi, KENYA.

For Passport photos in Nairobi CBD
Tel: +254 721 9000-27

         +254 0728 809 472